Mzee
nimebaini,
wana
wanaofanana,
Hawatiki
tofutini, wana mfanano wana,
Hawaji
tena mjini, maswala kuchanjiana,
Umangati
nauona, wangia kidedeani.
Acha
nikwelezeni, hali zino mzelewe,
Umangati
huno
nini,
na
kidedea
mjuwe,
Kinipata
makosani, niteteni nisiwawe,
Umangati
nauona, wangia kidedeani.
Nakumbuka
utotoni,
nilipokuwa
na
meno,
Nikiwa
kwetu nyumbani, kwa baba na mama Chano,
Nikifundwa
ya
ujani,
nilona
haya
maono,
Umangati
nauona, wangia kidedeani.
Nilifundwa
umangati, na mama pia na aba,
Si
wema niwe sifwati, katika la siku saba,
Kwani
huakupi
cheti,
kichora
itesha
raba,
Umangati
nauona, wangia kidedeani.
Umangati
huahidi, ahadi zilo kamili,
Huapisha
ikibidi,
ja
wa
Kwale
Mswahili,
Lakini
ngoma kurudi, ahadi kuitimili,
Umangati
nauona, wangia kidedeani.
Kisha
kuna kidedea, nifundishwa na wavyele,
Hiki
cheza
kuelea,
na
hurowa
kwa
utele,
Walinomba
kwendelea,
kizingatia
milele,
Umangati
nauona, wangia kidedeani.
Eti
kina kumanisha, wazaaji walinena,
Halafu
nisha wazisha, wankwisha ozeana,
Leo
nona
cha
kutisha,
kidea
kina
mikuna,
Umangati
nauona, wangia kidedeani.
Ino
mikuna naona, ni ile ya kimangati,
Ndo
mana
wazi
nanena,
kimengia
umangati,
Vipi
ikawezekana,
kushangaa
miye
sati,
Umangati
nauona, wangia kidedeani!!
Siddi
Kiroboto Mpole
“Mzee
Kimpole”
Kimpola
Language School,
Eldoret.
No comments:
Post a Comment