Tungo Za Kimpole
Saturday, 16 November 2013
Saturday, 28 September 2013
Page 1 of Mswahili Newsletter
Saturday, 4 May 2013
Wajinga wengi jamani
Mpole nimo chumbani, natunga nyingine tungo,
Namkosoa fulani, mwenye kusema uongo,
Vipi awe ukwelingi, hali amekuwa chongo,
Wengi wajinga jamani, wana radhi la ubishi.
Wana radhi la ubishi, wakianza hawasiti,
Mambo yao hayaishi, wanayo yenye risiti,
Kama kweli huwapishi, utaingia mashiti,
Wengi wajinga jamani, jepushe nao kiumbe.
Jepushe nao kiumbe, maisha haya mafupi,
Kama wataka utambe, utafumwa kwa rawapi,
Kesha kimya usiambe, kuamba kuna ukopi,
Wengi wajinga jamani, leo waitwa werevu.
Kama kusoma mama
Nasema nao wadama, mawakili wa kusoma,
Wanaosema daima, kusoma ni kwa lazima,
Nipeni bila kukoma, sababu zinowatuma,
Kama kusoma ni mama, nambie baba ni nani?
Nambie baba ni nani, tena jina lake lipi,
Ndipo none tumaini, la sivyo sifa sikupi,
Bila kusoma jamani, wengi wanazila pipi,
Kama kusoma ni mama, nambie baba ni nani?
Mama huzaa hakika, akalea na kuasa,
Bali baba atakika, kunapojiri mikasa,
Basi wenzi nawataka, baba pewe ukurasa,
Kama kusaoma ni mama, nipe babna nifaulu.
Nipe baba nifaulu, kitabu sio mkate,
Nenda hata kwa hikalu, wahubiri nwakute,
Siketi nigeke mbulu, kamili wapi nipate,
Sawa kusoma ni mama, baba njoo unitunge.
Malenga Sidi Kiroboto Mpole
Eldoret.
Thursday, 17 January 2013
Umangati wengia kidedeani!!!
Mzee
nimebaini,
wana
wanaofanana,
Hawatiki
tofutini, wana mfanano wana,
Hawaji
tena mjini, maswala kuchanjiana,
Umangati
nauona, wangia kidedeani.
Acha
nikwelezeni, hali zino mzelewe,
Umangati
huno
nini,
na
kidedea
mjuwe,
Kinipata
makosani, niteteni nisiwawe,
Umangati
nauona, wangia kidedeani.
Nakumbuka
utotoni,
nilipokuwa
na
meno,
Nikiwa
kwetu nyumbani, kwa baba na mama Chano,
Nikifundwa
ya
ujani,
nilona
haya
maono,
Umangati
nauona, wangia kidedeani.
Nilifundwa
umangati, na mama pia na aba,
Si
wema niwe sifwati, katika la siku saba,
Kwani
huakupi
cheti,
kichora
itesha
raba,
Umangati
nauona, wangia kidedeani.
Umangati
huahidi, ahadi zilo kamili,
Huapisha
ikibidi,
ja
wa
Kwale
Mswahili,
Lakini
ngoma kurudi, ahadi kuitimili,
Umangati
nauona, wangia kidedeani.
Kisha
kuna kidedea, nifundishwa na wavyele,
Hiki
cheza
kuelea,
na
hurowa
kwa
utele,
Walinomba
kwendelea,
kizingatia
milele,
Umangati
nauona, wangia kidedeani.
Eti
kina kumanisha, wazaaji walinena,
Halafu
nisha wazisha, wankwisha ozeana,
Leo
nona
cha
kutisha,
kidea
kina
mikuna,
Umangati
nauona, wangia kidedeani.
Ino
mikuna naona, ni ile ya kimangati,
Ndo
mana
wazi
nanena,
kimengia
umangati,
Vipi
ikawezekana,
kushangaa
miye
sati,
Umangati
nauona, wangia kidedeani!!
Siddi
Kiroboto Mpole
“Mzee
Kimpole”
Kimpola
Language School,
Eldoret.
Tuesday, 18 September 2012
Wanga wawa dume gani?!
Eddi nipelo sikizi, Mpole
nasema nawe,
Umegeuka kilizi, sababu
nomba nijuwe,
Una nini siku hizi,
tuambie tukijuwe,
Wanga wawa dume gani,
kulialia ja mwana.
Kulialia ja mwana, redioni
gazetini,
Kifo nani hataona, ndo
kijaze mdomoni,
Unawapotosha wana, toa
mfano mwanani,
Wanga wawa dume gani,
Mpole nakushangaa.
Mpole nakushangaa, malenga
wa Visramu,
Kijua umekomaa, kumbe bado
kuhitimu,
Ni bora ukinyamaa,
usidhaniwe wazimu,
Wanga wawa dume gani,
nahurumia mkeo.
Nahurumia mkeo, kwani
kulea hakomi,
Hamna aso upeo, acha
kuzitoa kemi,
Hujui kifo ni cheo, sio
cha mapeni kumi,
Wanga wawa dume gani,
wawasiwasika bure.
Wawasiwasika bure, hakuna
anokwandama,
Zikumbuke hamrere, kwa
wengi ulizotuma,
Ndizo zafanya uhare, pole
hutaki kusema,
Wanga wawa dume gani,
wanishangaza Mpole,
Wanishangaza Mpole, mie
mkongwe bondeni,
Wazileta siku zile, Kizere
kivuma ndani,
Uje kwangu tuselele, juma
zima mafunzoni,
Wanga wawa dume gani,
kulia achia wana.
Chombo kikitia nanga
Mzee ni ukumbini, na tabu
la ujanani,
Natia macho miwani,
nimsomee Fulani,
Maisha ya duniani, wangi
hawajui nini,
Chombo kikitia nanga, si
mwisho wa usafiri.
Si mwisho wa usafiri, hata
kama umefika,
Huishi kwenye bandari,
kwenda zaidi tataka,
Ipe mgongo bahari, na
uikabili njia,
Chombo kikitia nanga,
teremka kwa makini.
Teremka kwa makini,
uikague sehemu,
Jua lengo kuu nini, nakili
kwa tarakimu,
Kama ndipo ubaini, lau
sipo ufahamu,
Chombo kikitia nanga,
yasubiri maelezo.
Yasubiri maelezo, usanze
bure kuranda,
Yako kote matatizo, kokote
unakokwenda,
Hayakeri maulizo, wangi
mno mewalinda,
Chombo kikitia nanga,
usanze kutoa mali.
Usanze kutoa mali,
itatwaliwa haraka,
Ufikiri mara mbili,
uhakiki umefika,
Wanolipuuza hili, huchekwa
wanapotoka,
Chombo kkitia nanga,
sikiza yao wazee.
Sikiza yao wazee, kama
miye Kimpole,
Tukiteswa tutetee, radhi
tulinazo tele,
Acha nende waombee, Mola
awone milele,
Chombo kikitia nanga,
umkumbuke Rabuka.
Subscribe to:
Posts (Atom)